Conte asaka damu changa

Kocha wa Chelsea, Antonio Konte ameachana na mpango wa kumsajili kiungo wa Juventus, Claudio Marchisio na badala yake amesema anatafuta damu changa ili kuimarisha kikosi chake msimu ujao Licha ya kufanya kazi na Marchisio wakati akiwa kocha wa Juventus 'Old Lady', Antonio Conte alikuwa na matarajio ya kumchukua mchezji huyo katika kipindi hiki cha kiangazi. Mtandao wa Goal.com umeripoti kwamba kwa mujibu wa sera ya klabu hiyo kumsajili mchezaji wa miaka 32 ni kwenda kinyume na sera ya timu hiyo ambapo kwa sasa malengo ya klabu ni kununua wachezji walio chini ya miaka 30. Kutokana na uhakika wa timu hiyo kushiriki Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani, kocha huyo ameamua kukiimarisha kikosi chake mapema msimu huu wa kiangazi. Lich aya Marchisio kuwa na uzoefu mkubwa kutokana na kushiriki mashindano mbalimbali hata hivyo umri wake umekuwa kikwazo kutokana na sera za Chelsea. Kwa maana hiyo mchezaji huyo ataendelea kuwa kwenye mipango ya Kocha wake Massimiliano Allegri katika Uwanja wa Juventus. Hivyo Chelsea huenda ikageukia mpango wake wa kusajili vingo kama vile wa kutoka Monaco, Tiemouse Bakayoko na wa Atalanta, Frank Kessie. Wachezaji wote hao miaka yao inaendana na mipango ya Chelsea ambao wanatumia mfumo wa 3-4-3 ambao umeonekana kuwanufaisha na kuimarika kiwango chao kwa zaidi ya miezi siata sasa. Licha ya kuwapo na mpango wa kumsajili kiungo huyo ambaye mipango imegonga mwamba, pia Conte aanawawinda Victor Moses na Marcus Alonso katika msimu huu.

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii