Kwa Mara ya Kwanza, Dayna Nyange Anyakua Tuzo za Kimataifa

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/04/kwa-mara-ya-kwanza-dayna-nyange-anyakua.html
Dayna Nyange amekuwa Mtanzania pekee kuibuka mshindi wa Tuzo mbili za BAE Awards 2017zilizofanyika nchini Nigeria.
Dayna Nyange ameshibnda vipengele viwili ambavyo ni BEST AFRICAN ACT alichokuwa akichuana na Eddy Kenzo (Uganda), King Kaka (Kenya), Stoneboy (Ghana) pamoja na Jah Vinci (Jamaica).
Pia ameshinda Kipengele cha BEST VOCAL PERFORMANCE FEMALE kupitia wimbo wake ‘Angejua’ ambapo alikuwa akiwania tuzo hiyo na Aramide, Ngowari na Rocknana (wote kutoka Nigeria).
Ni kwa mara ya kwanza masanii huyo kuchaguliwa na kushinda tuzo za Kiamataifa baada ya kupata nafasi kwenye tuzo hizo nchini Nigeria.
Akielezea furaha yake baada ya kunyakua tuzo hizo Nyange amesema;
“Leo imekuwa siku yangu ya furaha sana sana sana, ningependa ni washukuru wotee mliokesha mkiniombea, mlikesha mkihamasisha, mlikesha mkinipigia kura. Hatimaye tumefanikiwa kutwaa tuzo zote mbili nchini Nigeria.
BEST VOCAL PERFORMANCE FEMALE
BEST AFRICAN ARTISTE
Nawashukuru sana mashabiki zangu, ahsanteni sana wadau wangu, ahsanteni sana Media zote, watangazaji, waandishi, na Ma Dj. Pia Namshukuru producer wangu Mr. Ttouch, shukrani kwa menejiment yangu na wasanii wenzangu.
Sote tuliacha kazi na tukafanya kazi moja tu na hatimaye matunda ni haya. Sijashinda mimi tu @daynanyange bali imeshinda Tanzania na Afrika kwa ujumla. JuhudiZimezaaMatunda. Mungu awabariki sana.” Alisema Dayna Nyange.