Mane azua hofu Liverpool

Winga wa Liverpool, Sadio Mane huenda ikawa mwisho wake kucheza msimu huu kutokana na hofu kutanda juu ya goti lake aliloumia mwishoni mwa wiki. Mane aliumia wakati Liverpool ikiwachapa watani wao Everton kwa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Anfield. Taarifa zinasema Mane alipata majeraha kwenye mguu jambo ambalo linaonyesha kwamba atalazimika kuwa nje kwa zaidi ya wiki sita. Ilieleza kwamba tathmini kamili ya tatizo lake litabainika baada ya uchunguzi wa kina. Hata hivyo timu ya wataalamu walishindwa kuanza kujua ukubwa wa athari kutokana na kupata maumivu makali. Taaifa hiyo ilisema, jambo la muhimu ni kujua kwamba watu wasiwe na wasiwasi kutokana na madhara aliyoyapata. Lakini sidhani kama kuna uwezekano wa Mane kuonekana tena uwanjani katika msimu huu. Hilo litakuwa ni pigo kubwa kwa Liverpool hasa katika kipindi hiki ambacho wanapambana kujiimarisha katika nafasi nne za juu.

Related

michezo na burudani 627112435447944868

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii