Nay adai kutishiwa maisha



Mwanamuziki Elibariki Emmanuel, maarufu kama
Mwanamuziki Elibariki Emmanuel, maarufu kama Nay wa Mitego 


 Mwanamuziki Elibariki Emmanuel, maarufu kama Nay wa Mitego amedai kutishiwa maisha na watu asiowafahamu baada ya kutumiwa ujumbe mfupi na kupigiwa simu wakimtaka ahame nchi kwa maelezo kuwa alichokifanya si kidogo.
Nay ambaye hivi karibuni alionana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe mjini Dodoma kwa ajili ya kujadili wimbo wake wa ‘Wapo’ alisema baadhi ya waliompigia simu walimtaka achukue tahadhari.
Alifafanua kuwa miongoni mwa ujumbe aliowahi kupokea ulisomeka kuwa; “Ulichokifanya sio kidogo na kuna watu hawako sawa na wanalifanyia kazi kuhakikisha wanakufundisha adabu, unatakiwa kuhama nchi uende ukakae huko hata mwaka mzima.”
Alisema baadhi ya watu wamemshauri abadili mtindo wa maisha ili aepuke kudhurika.
Kabla ya matukio hayo kumkumba, Nay alikamatwa na polisi akiwa kwenye onyesho mjini Morogoro kwa madai kuwa anaikashifu Serikali.
Siku moja baada ya kukamatwa, Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), liliufungia wimbo huo kwa madai kuwa hauna maadili.
Lakini siku hiyo hiyo, Waziri Mwakyembe alisema amezungumza na Rais John Magufuli ambaye amesema anaupenda wimbo huo.
Dk Mwakyembe alisema Rais ameruhusu wimbo huo kupigwa na ikiwezekana Nay auboreshe na atamuongezea baadhi ya mashairi.
Meneja wa Nay, Maneno John alidai ni kweli mwanamuziki huyo anatishiwa na ameshawahi kuona baadhi ya ujumbe wa simu, lakini hawajatoa taarifa polisi.     

Related

michezo na burudani 7931564911095023484

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii