Wapiga mbizi wamuokoa mwanamke

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/04/wapiga-mbizi-wamuokoa-mwanamke.html

Uhodari wa wapiga mbizi, umemuokoa abiria aliyekuwa akisafiri na Boti ya Kilimanjaro akitokea Dar es Salaam kwenda Zanzibar jana, baada ya kujitosa baharini saa 5:15 asubuhi.
Akielezea tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Hassan Nassir Ali alisema abiria huyo wa kike aliyetambuliwa kwa jina la Hudhaima Salum Abdulrahman (26), ni mkazi wa Kikwajuni Mjini Unguja.
Hassan alisema baada ya kuokolewa, alifanyiwa vipimo vya afya na mpaka jana jioni alikuwa akiendelea vizuri akiwa chini ya polisi.
“Tunaendelea na uchunguzi tukibaini kuwa huyu mwanamke alitenda kosa hilo kwa makusudi hatutomfumbia macho, lazima tutamfikisha mbele ya sheria ili ichukue mkondo wake,” alisema.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai baada ya abiria huyo kujitosa, walisikia sauti ikitokea baharini ya kutaka kuokoleawa.