Yanga kuupamba Muungano Dodoma




Yanga itapamba sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitakazofanyika kwa mara ya kwanza mkoani Dodoma kwa kucheza mechi na Kombaini ya Polisi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Jumatano.
Katibu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma(Dorefa), Hamiss Kissoy alithibitisha Yanga imekubali kucheza mechi hiyo ya kirafiki mkoani hapa.
Kissoy alisema Yanga inatarajiwa kuwasili mjini Dodoma kati ya leo jioni au kesho mchana tayari kwa mchezo huo.
“Tofauti na ilivyokuwa kwa Simba iliyocheza na
Polisi Dodoma pekee, kwa Yanga itacheza na timu ya Polisi Tanzania yenye muunganiko wa wachezaji kutoka timu za Jeshi la Polisi Tanzania kama vile Polisi Dodoma, Polisi Moro na Polisi Dar es salaam,” alisema Kissoy.
Viingilio vya mchezo huo Jukwaa Kuu V.I.P A itakuwa ni Sh10000 wakati V.I.P B Sh.5000 na Jukwaa la kawaida na mzunguko ni Sh3000.
Yanga itacheza Dodoma kwa mara ya kwanza tangu 2014 ilipocheza mechi ya kirafiki dhidi ya CDA kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini hapa.

Related

michezo na burudani 3793943451919089058

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii