Bunge lafuta maneno kwenye hotuba ya Sugu kabla ya kusomwa




Mbunge wa Mbeya mjini,  Joseph Mbilinyi 'Sugu'
Mbunge wa Mbeya mjini,  Joseph Mbilinyi 'Sugu' 

Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu ameagiza Hotuba ya Kambi ya Upinzani kuhusu Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ihaririwe na kufuta maneno yote katika kurasa 17.
Zungu ametoa uamuzi huo leo asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu, hata kabla ya bajeti yenyewe kuwakilishwa na Waziri Dk Harrison Mwakyembe.
Zungu amesema amezipitia hotuba zote na kubaini kuwa ile ya upinzani itakayowasilishwa na Joseph Mbilinyi 'Sugu' ina masuala yaliyopo mahakamani ambayo yamekwishazuiliwa katika bajeti zilizotangulia.
Amesema maneno yenye mwelekeo huo yakisomwa atachukua hatua.

Related

kitaifa 232174296552848468

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii