ligi bora inazaa Stars bora

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/05/ligi-bora-inazaa-stars-bora.html

Rishard amesema ushindani wa kweli ndiyo utakaozalisha wachezaji ambao wataleta maendeleo kwenye timu ya taifa vinginevyo kitakachokuwa kinafanyika ni pata potea.
"Kuna wakati ambapo makocha wanaweza kubeba lawama ambazo haziwahusu, ligi inaendelea na kila mtu anakiona kinachofanyika na wachezaji ambao wataitwa kwa ajili ya michuano ya CHAN na AFCON ni hao, hao na siku akikosekana Mbwana Samatta, Watanzania wanaona ndiyo basi tena," anasema nyota huyo ambaye alikuwepo kwenye kikosi cha Stars kilichoshiriki michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 1980.