Trump asisitiza hachunguzwi na FBI




Rais wa Marekani Donald Trump amesema hachunguzwi  na mtu yeyote wala shirika la ujasusi la FBI halimchunguzi. Hiyo ni baada ya kumfuta kazi mkurugenzi wa shirika la FBI.
Akizungumza na chombo cha habari cha NBC jana, Trump alisema  kwamba ilikuwa uamuzi wake pekee kumsimamisha kazi James Comey.
Comey alikuwa akiongoza uchunguzi kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani uliokamilika mbali na uwezekano kwamba kulikuwa na mawasiliano kati ya maofisa wa Trump na Urusi wakati wa kampeni.
Trump ameutaja uchunguzi huo kuwa unafiki mkubwa madai yaliyopingwa na mrithi wa Comey.
Katika mahojiano yake ya kwanza tangu alipomfuta kazi mkurugenzi huyo, Trump aliiambia NBC siku ya Alhamisi kwamba alimuuliza Comey iwapo alikuwa akimchunguza.
“Nilimwambia iwapo inawezekana unaweza kuniambia, Je Ninachunguzwa? Aliniambia, huchunguzwi.” alisema Trump


Related

kimataifa 6413837810633023393

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii