Rodriguez avurugwa Real Madrid
 
http://maisharaisi.blogspot.com/2017/06/rodriguez-avurugwa-real-madrid.html

 Kocha Jose Pekerman amesema kitendo cha uongozi wa Real Madrid kutomkubali James Rodriguez licha ya kuonyesha kiwango cha juu, kimemvuruga mchezaji huyo.
Hata hivyo, mchezaji huyo raia wa Columbia, kocha wa timu yake ya Taifa, Pekerman amekuwa akimwamini, lakini ameshangazwa kutopewa kipaumbele kwenye klabu yake.
Mchezaji huyo ameonekana kutopewa kipaumbele kwenye kikosi hicho cha Santiago Bernabeu, huku akikosekana kwenye kikosi kilichocheza fainali ya Ligi ya Mabingwa wiki iliyopita.
