Wadau wataka mabadiliko Tff.

Kocha Adolph Rishard amesema anamuunga mkono Ally Mayay aliyechukua fomu ya kugombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kwani anatosha katika nafasi hiyo. Mayay amerudisha fomu leo za kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa TFF utakaofanyika Agosti 12 akichuana na Jamal Malinzi, Athumani Nyamlani, Frederick Mwakalebela, Imani Madega, Wallace Karia na Fredrick Masolwa. Rishard alisema yeye pamoja na wachezaji wa zamani wanamuunga mkono Mayay na wanaamini akipata nafasi hiyo ataliongoza vema shirikisho hilo na kuupeleka mbele mpira wa Tanzania Alisema hawamuungi mkono Mayay kwa kuwa alicheza mpira zamani bali ana sifa zote za uongozi na ndio maana wameona anatosha katika nafasi hiyo. "Siyo kama anafaa kuiongoza TFF kwa sababu amecheza mpira, hapana ila ana uwezo mkubwa wa uongozi na ana nidhamu. "Ana elimu, amewahi kupata uongozi katika sehemu mbalimbali kama chuo, Yanga na kwingineko hivyo kwa uzoefu wake alioupata huko tumeona kuwa anafaa pia kuongoza hata TFF," alisema Rishard. Alisema pia Mayay analijua soka vizuri kwani licha ya kucheza kipindi cha nyuma, pia ni mchambuzi wa soka. Katika nafasi ya makamu wa rais waliochukua fomu mpaka sasa Mulamu Nghambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na Mtemi Ramadhan.

Related

michezo na burudani 2944425759390090859

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii