Singida United yatambulisha basi lao jipya




 Klabu ya Singida United imetambulisha ramsi basi lake jipya itakalotumia kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Basi hilo lenye thamani ya Sh 350 milioni limezinduliwa rasmi na litaanza kutumika katika safari za timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu.
Katika basi hiyo, Singida imeweka picha za Rais wa timu hiyo, Mwingulu Nchemba ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani pamoja na picha ya mmiliki wa timu, Yusuf Mwandami.
Ofisa Habari wa timu hiyo, Festo Sanga alisema wataanza maandalizi yao hivi karibuni ili kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu huku wakitarajia kukamilisha usajili wa nyota wachache waliosalia

Related

michezo na burudani 9076841301284264378

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii