Waziri Mkuu azindua zahanati ya kisasa Lindi










 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Shirika la Nyumba (NHC) kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Mnolela, Lindi kwa muda mfupi.
Amesema ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa umekamilika, jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo na wa jirani.
Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mnolela baada ya kuzindua zahanati hiyo iliyosimamiwa na NHC.
Amesema ujenzi wa zahanati hiyo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali wa kuboresha huduma za afya kwa kusogeza huduma karibu kwa wananchi wake.
“Rais wetu Dk John Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi changamoto mbalimbali zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa NHC,  Nehemia Mchechu amesema mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo ulisimamiwa na NHC na umegharimu Sh 65.5 milioni.
“Shilingi 15 milioni zimetolewa na Rais, Sh 10 milioni zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye, NHC imetoa  milioni 10 na kiasi kilichosalia ni mchango wa halmashauri,” amesema Mchechu
Awali Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape alimshukuru Rais Magufuli kwa mchango mkubwa alioutoa katika mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo.
Nape amesema zahanati hiyo ni mkombozi kwa wakazi wa kijiji cha Mnolela na wananchi wengine wanaoishi maeneo yaliyo jirani na kijiji hicho.

Related

kitaifa 4628706964230294624

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii