Utafiti: Watoto wasivyoweza kufanya majaribio ya darasa la pili

http://maisharaisi.blogspot.com/2018/02/utafiti-watoto-wasivyoweza-kufanya.html
Utafiti: Watoto wasivyoweza kufanya majaribio ya darasa la pili
Asilimia 38 ya watoto wenye umri wa miaka kati ya tisa na 13 nchini hawawezi kufanya majaribio ya darasa la pili.
Hayo ni matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi ya Twaweza leo Februari 27, 2018 uliowahusisha watoto 197,451 kutoka katika shule za msingi 4,750.
Akitoa matokeo ya utafiti huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze amesema kukosa usawa katika kujifunza ni changamoto nchini.
Amefafanua kuwa katika utafiti huo uliofanyika mwaka 2015, asilimia 75 ya watoto wa umri huo wana uwezo wa kufaulu wakati Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora ni asilimia 17.
Amesema tofauti hizo zinaonyesha kwamba eneo analoishi mtoto lina mchango mkubwa katika kujifunza.
Eyakuze amesema asilimia 42 ya watoto kutoka kaya maskini walifaulu majaribio ikilinganisha na asilimia 58 ya watoto kutoka katika kaya zenye uwezo.
Amesema matabaka haya yanajitokeza kwenye jamii hali ambayo ikiachwa iendelee inaweza kuwaacha maskini wakaendelea kuwa maskini.
Pia, amebainisha kuwa asilimia 74 ya watoto kati ya watatu hadi wanne ambao mama zao wana elimu ya sekondari au ya juu walifaulu majaribio matatu ikilinganishwa na asilimia 46 ya watoto ambao mama zao hawakusoma.
Majaribio hayo yalikuwa katika masomo ya kusoma Kiingereza, Kiswahili na kufanya hesabu rahisi