Wapinzani wa Yanga wapigwa 3-1 mchezo wa Ligi Kuu




Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania,Rashid Mandawa anayeichezea BDF XI amefunga usiku wa jana mabao matatu (hat trick) dhidi ya wapinzani wa Yanga, Township Rollers kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini Botswana (BWPL).
Mandawa alifunga mabao hayo dakika ya  20,39 na 45 Katika mchezo huo ambao BDF XI  iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani, Molepolole Stadium.
Akizungumzia mabao hayo muhimu ambayo yameipa pointi tatu BDF XI, Mandawa amemshukuru Mungu kwa kumuwezesha kupachika mabao hayo.
“Sio kitu chepesi kuwafunga mabingwa watetezi katika michezo yote miwili,ukiachilia mbali haya mabao matatu pia katika mzunguko wa kwanza niliwafunga bao moja japo tulipoteza kwa mabao 3-2,” alisema Mandawa.
Hat trick hiyo imemfanya mshambuliaji huyo wa zamani wa Kagera Sugar kufikisha jumla ya mabao 11 huku akitengeneza mengine matano kwenye michezo 19 ya BWPL.






Related

michezo na burudani 1487949333308782012

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii