Mahakama yaamuru Seth kutibiwa Muhimbili

http://maisharaisi.blogspot.com/2018/03/mahakama-yaamuru-seth-kutibiwa-muhimbili.html

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Machi 28, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi baada ya mshtakiwa huyo kujieleza mahakamani hapo kuwa afya yake siyo nzuri hivyo anaomba kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
"Mshtakiwa anaonekana hata kwa macho, hivyo naamuru mshtakiwa huyu apelekwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, akapatiwe matibabu ili kesi yake itakavyokuja kuendelea awe na afya nzuri ," amesema hakimu Shahidi.
Mbali na Seth, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara, James Rugemarila ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 katika Mahakama hiyo.
Awali wakili wa Takukuru, Pendo Temu akisaidiana na Leonard Swai alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa shauri bado haujakamilika.
Katika kesi ya msingi, washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Sh309 bilioni.