Miguna Miguna arejea Kenya na makeke yake




Mwanasheria machachari na aliyejitangaza kuwa jenerali wa Vuguvugu la Taifa Kuipinga Serikali (NRM), Miguna Miguna amerejea nchini akitokea London, Uingereza ambako aliwekwa kizuizini kwa saa tatu.
Miguna ametua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi baada ya kukaa kwa wiki sita Canada ambako alirejeshwa. Ndege aliyopanda ya Shirika la Emirates imetua saa 8:30 alasiri ambako alipokewa na wanasheria wake.
Mwanasheria wa Miguna, Cliff Ombeta amesema waliamriwa kusalimisha hati ya kusafiria ya Canada lakini waligoma.
Mkasa wa Uingereza
Ilikuwa Alhamisi jioni wakati gazeti la Nation lilipofika Uwanja wa Ndege wa Heathrow (Uwanja Na 2), ili kuhabarisha kuwasili kwa Miguna Miguna aliyetarajiwa kutua Uingereza.
Kila kitu kilikuwa kimekwenda sawa hadi ndege iliyokuwa imembeba jenerali wa NRM ilipotua ikitokea Ujerumani pamoja na abiria wengine.
Abiria wote ambao safari zao zilikuwa zinaishia katika nchi ile ya Malkia, isipokuwa Miguna walitoka nje ya uwanja na kuondoka.
Muda mfupi baadaye, mwanasheria huyo machachari alituma ujumbe kupitia mtandao wa WhatsApp kuwajulisha wenyeji wake waliokuwa wakimsubiri nje kwamba amesubirishwa na maofisa polisi wa Uingereza wanaohusika na uhamiaji. Idhini yake, alisema ilitakiwa kusubiri ikiwa ataruhusiwa kuendelea au la.
Miguna alisubiri kwa muda wa saa tatu tangu alipowasili kwenye uwanja wa ndege. Baadaye aliruhusiwa kuendelea na ziara yake ya NRM katika miji ya Oxford na London.

Related

kimataifa 235052706080669736

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii