Diamond alikoroga tena, picha za video chumbani hatarini kumpandisha kizimbani



Mwanamuziki Nassib Abdul maarufu Diamond Platnumz ameingia katika mgogoro mwingine na vyombo vya dola na safari hii huenda akakabiliwa na faini au kifungo kisichopungua miaka saba iwapo atafikishwa mahakamani na kupatikana na hatia.
Diamond alihojiwa na polisi juzi kuhusu tuhuma za kusambaza picha kinyume na maadili na baadaye rapa Billnass na mwanamitindo Hamisa Mobeto kuhojiwa kuhusu tuhuma kama hizo huku mwanamuziki Nandy akisakwa baada ya wasanii kuonekana kwenye video mbili zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonyesha kama watu walio katika faragha.
Kamanda wa polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema mwanamuziki huyo alikamatwa kwa tuhuma za kufanya kosa la mtandao kwa kupiga picha za utupu na kuzisambaza.
“Amekamatwa jana (juzi) na kuhojiwa. Baada ya kuandika maelezo amepata dhamana na kuachiwa. Tunaendelea na upelelezi pale utakapokamilika atafikishwa mahakamani,” alisema Mambosasa.
Alisema makosa hayo ni kinyume na sheria za nchi pamoja na maadili, hivyo amekamatwa na kuhojiwa kama watuhumiwa wengine na kwamba kitendo cha kusambaza picha zisizo na maadili hakikubaliki.
Kamanda Mambosasa aliwataka wasanii na watu maarufu kutii sheria za nchi bila kushurutishwa.
Habari hizo zilitinga bungeni jana baada ya mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga kutaka kujua Serikali ina mkakati gani kukomesha tabia za baadhi ya watu wanaotumia mitandao vibaya ikiwemo kuhamasisha masuala ya ushoga.
Akijibu swali hilo la nyongeza, waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alilitaarifu Bunge kuwa mwimbaji huyo nyota wa kibao cha “Number One” alikamatwa juzi kwa tuhuma za kusambaza picha zilizokosa maadili mitandaoni.
Mbali na hilo, Dk Mwakyembe aliagiza Nandy asakwe na kufikishwa katika mikono ya sheria kwa tuhuma kama hizo baada ya video yake kusambaa mitandaoni wiki iliyopita. Tayari Nandy amewaomba radhi mashabiki wake kwa kitendo hicho.
Katika mitandao ya kijamii juzi, video inayomuonyesha Diamond akiwa na wanawake wawili faraghani ilisambaa na kuibua mijadala mikubwa kuhusu nyota huyo ambaye mwezi uliopita alikuwa na mgogoro na wizara hiyo kutokana na kauli yake dhidi ya naibu waziri, Juliana Shonza.
Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 inamzuia mtu yeyote kuchapisha au kusababisha kuchapisha kwa kutumia kompyuta picha za ngono au matukio ya faragha ambayo hayapaswi kuonekana.
Pia sheria hiyo inasema atakayekiuka atakuwa na hatia ya kuhukumiwa kifungo kisichopungua miaka saba au faini ya Sh20 milioni au vyote kwa pamoja.

Related

michezo na burudani 7475335077707908903

Post a Comment

  1. Caesars Rewards Club | Casino & Poker Rewards
    Play poker, blackjack, and 영주 출장안마 more with the rewards club. 보령 출장샵 Discover rewards, loyalty points, and other 대전광역 출장마사지 rewards you 제주도 출장마사지 can 화성 출장안마 use to earn rewards from poker and casino

    ReplyDelete

emo-but-icon

item
Kicbjamii