Ndalichako ajitetea ripoti ya CAG


 Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako, amesema anaitumia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kama changamoto na chachu ya kuendelea kufanya kazi nzuri.
 Ndalicho ameyasema hayo jana Aprili 17 wakati akijibu hoja za ripoti ya CAG iliyosomwa wiki iliyopita bungeni.
 Wiki iliyopita mawaziri wanane walifanya mkutano na waandishi wa habari wakijibu hoja za ripoti ya CAG.
“Serikali ya awamu ya tano kwenye suala la udhibiti haina utani kila mtu ameona kazi ambayo imefanyika, tunapopata ripotri ya CAG, inatupa chachu ya kuendeleza na kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano,” amesema
Amesema kama CAG alivyoshauri, watafanyia kazi mapendekezo ya CAG na pia watawachukulia hatua watendaji wanaotumia vibaya fedha za umma.
Ndalichako alizungumzia hoja ya CAG kuhusu ukusanyaji hafifu wa fedha za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na akasema, tangu serikali ya awamo ya tano iingie madarakani, kumekuwa na ongezeko la ukusanyaji wa madeni hayo.
“Taarifa ya CAG 2015/16 hadi 2016/17    inaionyesha kuwa makusanyo yameongezeka kutoka Sh28bilioni hadi Sh 116bilioni. Hilo ni ongezeko la asilimia 300. Takwimu hazidanganyi,” amesema
Hata hivyo amesema bado makusanyo hayo hayatoshelezi na ameitaka  Menejimenti ya Bodi ya Mikopo kuhakikisha ukusanyaji wa mikopo unaimarishwa.

Related

elimu 1819366160732772855

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii