Kocha wa tatu kutua mbao fc



Klabu ya Mbao imeongeza nguvu katika benchi la ufundi kwa kumchukua kocha Fulgence Novatus ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha timu hiyo inakwepa janga la kushuka daraja msimu huu .
Novatus ambaye alikuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa ‘Taifa Star, alitua kikosini humo na alitarajia kuanza kazi jana. Kutua kwa Novatus kunalifanya benchi la ufundi la timu hiyo kufikisha Makocha watatu, akiwamo Ettiene Ndayiragije (Kocha Mkuu) na Ahmad Ally ambaye ni Msaidizi.Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Solly Njashi alisema wameamua kuon-geza nguvu ili kuhakikisha timu ina-fanya vizuri na kubaki Ligi Kuu.
“Tumeamua kuongeza nguvu kwenye Benchi la Ufundi kwa kumu-weka Fulgence (Novatus)ambaye ataanza kazi leo (jana), lengo ni kuhakikisha timu inafanya vizuri na kukwepa janga la kushuka daraja,” alisema Njashi. (Saddam Sadick)

Related

michezo na burudani 65104318692709118

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii