Roma yauza tiketi za mechi Liverpool kabla ya droo ya leo



 AS Roma imetoa kali ya mwaka baada ya kuchapisha tiketi ya nusu fainali Ligi Mabingwa kuwa watacheza na Liverpool kabla ya kupangwa kwa ratiba mechi hiyo leo mchana.
Miamba hiyo ya Italia wamefanikiwa kutinga kwa nusu fainali  ya mashindano hayo kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo baada ya kuiondoa Barcelona katika robo fainali.
Mafanikio hayo yamewafanya kuchapisha tiketi na kuwataka mashabiki wake wanunua katika mchezo wao wa nyumbani dhidi ya vijana wa Jurgen Klopp.
Makosa hayo yaliyofanywa katika tovuti ya klabu hiyo yaliondolewa haraka baadaye, lakini tayari baadhi ya mashabiki walikuwa wamefanikiwa kupiga picha ‘screenshot’ tiketi hiyo inayoonyesha mechi hiyo itachezwa Mei 2.
Ratiba ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa itapangwa leo Ijumaa mchana huu Uswisi.
Timu nyingine zilizoingia kucheza hatua hiyo ni pamoja na mabingwa watetezi Real Madrid na vigogo wa Ujerumani, Bayern Munich wote wanasubiri ratiba hiyo.

Related

michezo na burudani 4122019609197262290

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii