NGORONGORO HEROES KUWAFUATA DR CONGO,MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO WAJITOKEZA KUIDHAMINI


Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Kikosi cha Wachezaji 21 na Viongozi 7 wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes waliondoka usiku wajana kuelekea DR Congo kwenye mchezo wao wa marudiano wa kufuzu fainali za Africa kwa Vijana dhidi ya Timu ya taifa ya Vijana ya DR Congo safari iliyodhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Ngorongoro Heroes inaondoka kwa kutumia Shirika la Ndege la Ethiopia ambapo leo wanatarajia kufanya mazoezi kuelekea mchezo huo utakaochezwa Jumapili Aprili 22,2018.Ikumbukwe mchezo wa awli wlitoka  suluhu ya bila kufungana  uwanja wa taifa  dar-es-salaam

Naye Kocha Mkuu wa Ngorongoro Heroes Ammy Ninje amesema maandalizi yanaridhisha na vijana wamepokea vyema mafundisho yake ikiwemo mfumo mpya wa namna ya kucheza na DR Congo ugenini.
Ninje amesema wanafahamu kazi iliyopo mbele yao lakini kwa maandalizi yaliyofanyika imani ni kubwa ya kufanya vizuri wakichagizwa na udhamini wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambao wamejitokeza kuisafirisha timu hiyo jambo ambalo linawatia nguvu zaidi.
Nahodha wa kikosi hicho Issa Makamba amesema wachezaji wako tayari kwenda kuwakilisha vyema na wametiwa hamasa kubwa zaidi na morali kutoka kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Amesema wao vijana kazi yao ni moja kufanya vizuri kwenye mchezo huo kwa kupata matokeo yatakayowapeleka kwenye hatua ya raundi ya pili.

Related

michezo na burudani 269865995493841949

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii