Mwigulu atoa agizo zito kwa polisi Pwani




Kibaha. Jeshi la Polisi nchini limeelekezwa kuanzia sasa liwashughulikie kwa uzito unaostahili wahalifu wa makosa makubwa ikiwemo ugaidi, ushoga, mauaji na uvamizi wa kutumia silaha ili kama wapo wengine wanaotaka kujihusisha na matukio hayo wakome.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa maelekezo hayo leo akizungumza na maofisa pamoja na askari zaidi ya 200 wa majeshi yote yaliyopo chini ya wizara hiyo mkoani Pwani  na kuelekeza  kamwe wasicheze na wahalifu wa matukio hayo tena bali wawatie adabu sawasawa.
Alisema wakati tunaelekea katika Jeshi la kisasa lazima hata kiutendaji mambo nayo yaende kisasa zaidi katika kuyashughulikia makosa ya aina hiyo pamoja na wa dawa za kulevya, mimba kwa wanafunzi na ubakaji lazima nayo yashughulikiwe kwa namna tofauti kabisa ili yasiwe yanajirudia hovyo kwa jamii.

Related

maisharaisi 8479576349617664141

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii