RAISI MAGUFULI AFANYA UTEUZI KWAMARANYINGINE TENA.



Dar es Salaam. Rais John Magufuli amewateua wakuu wa wilaya wawili na wakurugenzi watatu wa Mamlaka za Serikali za mitaa na wenyeviti saba wa Bodi za taasisi za Serikali kujaza nafasi zilizokuwa wazi.
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi ilisema Rais Magufuli amemteua Kisare Makori kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo katika Mkoa wa Dar es Salaam kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Humphrey Polepole aliyeteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi.
“Uteuzi huu unaanza mara moja na wateule wote wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) mara wapatapo taarifa hii,” alisema Balozi Kijazi katika taarifa hiyo.
Wengine ni Evod Mmanda aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Khatib Kazungu aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango; na Ramadhan Geofrey Mwangulumbi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Lewis Kalinjuna aliyestaafu kwa mujibu wa sheria.

Related

siasa 8922321040657302404

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii