Aomba washtakiwa wa samaki waachiwe

https://maisharaisi.blogspot.com/2017/02/aomba-washtakiwa-wa-samaki-waachiwe.html
Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani jana, lakini hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu korti hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.
Wakili Mkumbe alidai kuwa shauri hilo lilishaamuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Januari 24, baada ya kutumia Sheria ya Forodha kutaifisha magari matatu ya watuhumiwa, samaki na mshtakiwa wa kwanza Joseph Mushi kutozwa faini ya Sh3.97 milioni.
Waliofikishwa kizimbani jana ni wafanyabiashara wawili wa samaki jijini Mbeya, Joseph Mushi, Said Ramadhan, maofisa watatu wa TRA Kituo cha Tunduma; Andrew Ngachengo, Ibrahim James na Lugano Mwakapala.
Wengine ni wakala wa mpakani mwa Tanzania na Zambia upande wa Tunduma, Agripa Benjamin, Shaaban Sankwa, Said Sisige na Pius Joseph ambao ni madereva wa magari yaliyokutwa na shehena ya samaki.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite alisema jalada la kesi litafikishwa Mahakama Kuu leo. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 7.