TCU, changa la macho





 Uongozi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (Saut), umesema baadhi ya wanafunzi walioorodheshwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuwa taarifa zao za uhakiki zina kasoro hivyo kuwa hatarini kukosa sifa za kuendelea na masomo, walishamaliza masomo zaidi ya miaka mitatu iliyopita.
Mbali na kauli hiyo, chuo hicho, vyuo vingine vya elimu ya juu na wadau wa elimu wameijia juu TCU wakisema taasisi hiyo ndiyo inayopaswa kubeba lawama.
Juzi, TCU ilitoa orodha ya vyuo 52 ambavyo ilidai wanafunzi wake walidahiliwa katika masomo ambayo hawakustahili na kutoa muda hadi Februari 28 kufanya uhakiki vinginevyo watapoteza sifa za uanafunzi.
Lakini jana, uongozi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine ulisema Serikali ndiyo inayopaswa kuwajibika.
Makamu Mkuu wa Saut ambacho kimetajwa kuwa na wanafunzi 1,046 wasiokidhi vigezo, Dk Thadeus Mkamwa alisema kuwa chuo hicho kilifuata taratibu zote lakini wameshangaa TCU ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kudahili wanafunzi, kutoa taarifa zenye mkanganyiko.



Related

elimu 7694528780788262357

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii