Mimba zafifisha elimu





Takriban wasichana 40  wanaofaulu kuendelea na kidato cha kwanza katika Sekondari ya Mkirira wilayani hapa, huacha shule kila mwaka kutokana na mimba.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Sekondari ya Nyengina juzi, Mwenyekiti wa Umoja wa Maendeleo wa Watu wa Bukwaya (Umabu), Robeta Masinde alisema umbali mrefu wa kufika shuleni unachochea hali hiyo.
Masinde alimuomba Mbunge wa jimbo hilo, Profesa Sospeter Muhongo kununua gari la wanafunzi ambalo wazazi watachanga fedha za mafuta na posho ya dereva.
Hata hivyo, Profesa Muhongo alisema hatatoa gari la wanafunzi hadi viongozi watakapotengeneza magari ya kubebea wagonjwa aliyotoa miaka iliyopita.

Related

elimu 8403947474770019107

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii