Utendaji wa maofisa ugani kudhibitiwa.

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/01/utendaji-wa-maofisa-ugani-kudhibitiwa.html
Hai. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Sadiki amewataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuwasimamia maofisa ugani ili wawasaidie wakulima wa kahawa kutumia miche bora.
Sadiki alisema maofisa hao wana wajibu wa kuwasimamia wakulima na kuwaelekeza kutumia miche inayozalishwa na Kituo cha Utafiti wa Kahawa (Tacri) ili kulirejesha zao hilo katika hali yake ya zamani.
Mkuu huyo wa mkoa alisema hayo jana alipokitembelea kituo hicho kinachozalisha aina 19 ya miche bora ya kahawa ambayo haishambuliwi na magonjwa.