Kangomba’ yawapeleka sita mahabusu.

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/01/kangomba-yawapeleka-sita-mahabusu.html

Mtwara. Polisi mkoani Mtwara inawashikilia watu sita, wakiwamo wawili wenye asili ya Kiasia wakiwa na magari mawili yenye tani 29 za korosho walizokuwa wakijaribu kuziingiza bandarini ili zisafirishwe kwenda nje.
Korosho hizo zinasadikiwa kununuliwa nje ya mfumo wa stakabadhi ghalani maarufu kama ‘kangomba’ ambao humpunja mkulima, kukosesha halmashauri mapato na Taifa.
Watu hao walikamatwa bandarini juzi saa mbili usiku wakiwa na vielelezo vinavyodaiwa kuwa bandia baada ya askari wa Bandari ya Mtwara kuvitilia shaka.