Wanafunzi 55,000 kupatiwa chakula shuleni





Arusha. Zaidi ya wanafunzi 55,000 kutoka shule 48 za msingi katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, wanatarajia kunufaika na mpango wa chakula shuleni unaolenga kuinua kiwango cha ufaulu.
Mpango huo wa bila masharti unatarajia kuanza kutekelezwa mwezi huu na kukamilika mwishoni mwa mwaka kwa usimamizi wa halmashauri ukifadhiliwa na wadau mbalimbali.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Athuman Kihamia alisema juzi kuwa pia mpango huo utaongeza mahudhurio ya wanafunzi shuleni kwa kuwa wamebaini huathiriwa na njaa.


Related

maisharaisi 8672967327107395731

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii