Wabunge wahofia Serikali kushindwa kuufanya uchumi kuwa wa viwanda





Mwenyekiti wa kamati ya Viwanda, Biashara na
Mwenyekiti wa kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Dk Dalaly Kafumu 

Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imesema hali ya kibajeti inaashiria Serikali kushindwa kutekeleza azma yake ya kuufanya uchumi wa Tanzania kuwa wa viwanda.
Wabunge walisema hayo jana wakati wakichangia ripoti ya wizara ya Viwanda na Biashara iliyowasilishwa  bungeni.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Dalaly Kafumu alisema mwaka 2016/2017, Serikali iliongeza bajeti ya maendeleo ya wizara hiyo kutoka Sh35.3 milioni hadi Sh42.1 milioni.
“Ongezeko hili lilikuwa ni sawa na asilimia 16.06 ya bajeti ya mwaka 2015/2016. Lakini cha kusikitisha Serikali imeshindwa kutoa fedha zilizopitishwa na Bunge kwa wizara hiyo kwa wakati,” alisema.
Dk Kafumu, ambaye pia ni mbunge wa Igunga (CCM), alisema kutokana na hali hiyo azma ya Serikali ya kufikia uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025 inaweza kuwa ndoto.
Mwenyekiti huyo alisema hadi kufikia robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2016/2017, wizara hiyo ilikuwa haijapokea kiasi chochote cha fedha ya bajeti ya maendeleo.
“Wizara imepokea Sh7.6 bilioni tu sawa na asilimia 18.6 ya fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa mwaka 2016/2017. Hali siyo nzuri na inaashiria Serikali kushindwa kutekeleza azma yake ya kutekeleza miradi mingi ya maendeleo kama ilivyokuwa imepanga kwa mwaka wa fedha 2016/2017,” alisema.




Related

kitaifa 9200115059815284322

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii