Tabora kusikiliza kero za wananchi kila wiki



 Urambo. Wakati Mkoa wa Mbeya ukitenga Alhamis(Jana)  kwa kila wiki kuwa ya wakuu na wakurugenzi watendaji wa wilaya kusikiliza kero za wananchi ikiwamo ardhi, Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora ametoa agizo kwa watendaji.
Mkuu huyo wa wilaya, Angelina Kwingwa amewataka watumishi wa Idara ya Ardhi kupunguza migogoro ya ardhi vinginevyo wajitathmini kama wanafaa kuendelea kuwapo kazini.
Akizungumza na watendaji wa halmashauri, Kwingwa alisema kuna migogoro mingi ambayo imezidi katika kata za wilaya hiyo, huku Kata ya Imalamakoye ikiwa ni kinara.
Alisema ni lazima migogoro hiyo ipunguzwe kama au kumalizwa kabisa kwani ni kero kubwa kwa wananchi.
“Kila siku ofisi ya mkuu wa wilaya kuna foleni ndefu ya watu wanaofika kuwasilisha malalamiko yao na yote yanahusu ardhi, ni lazima watumishi wa idara hiyo mjitathimini na muanze kushughulikia tatizo hilo mara moja,” alisema Kwingwa.
Pia, aliwataka watendaji hao kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano na kuwasihi kukutana nao wananchi ili wazungumze suala hilo.
Mbunge wa Urambo, Magreth Sitta alisema migogoro mingi inatokana na wananchi kutopewa elimu kuhusu mabadiliko ya ardhi na kwamba, watumishi wanapaswa kuwaelimisha wananchi.
Mbunge huyo alisema kama wananchi hawapewa elimu ya kuepuka migogoro ya ardhi haitakwisha kwa kuwa wengi huisababisha kutokana na kukosa elimu.
“Mimi mwenyewe ardhi yangu ilichukuliwa, lakini baada ya kuelimishwa na kuzungumza na wahusika na nyinyi watumishi toeni elimu kwa wananchi,” alisema.
Mkazi wa mjini hapa, Elisha Butonja alisema  migogoro mingi inatokana na wananchi kuuza mara mbili maeneo yao na viwanja kugawiwa zaidi ya mara moja.

Related

kitaifa 1287360501295477697

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii