Hospitali ya rufaa mkoa wa mbeya yapokea msaada wa mashuka

Chama cha Akiba na Mikopo cha Lulu kimetoa msaada wa mashuka 200 kwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya ili kukabiliana na upungufu uliopo. Mwenyekiti wa Bodi ya Lulu Saccos, Vitus Kibasa alisema pia wametoa msaada wa aina hiyo kwenye hospitali nyingine mkoani humo. Akipokea mashuka hayo juzi, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk Agness Buchwa alisema Hospitali ya Rufaa ya Mbeya inaupungufu wa mashuka 640. “Hospitali hii inahitaji misaada mingi ikiwamo kujenga miundombinu hususan wodi za wazazi, njia za kupitisha wagonjwa, vitanda na vitendea kazi vingine,” alisema.

Related

kitaifa 8173325330026664868

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii