Kabunda mchezaji bora mwezi wa pili

Kiungo wa Mwadui FC, Hassan Kabunda amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa Februari. Kabunda aliwashinda washambuliaji wawili wa Simba, Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib. Katika mechi tatu alizoichea Mwadui mwezi huo, Kabunda alicheza kwa dakika zote 270 na kuisaidia timu yake kukusanya pointi sita zilizoifanya ipande kwa nafasi mbili katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya nane hadi ya sita. Kabunda alifunga jumla ya mabao manne katika mechi hizo tatu kati ya sita iliyofunga timu yake. Kiungo huyo alionyesha nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopata onyo lolote la mdomo au kadi kutoka kwa waamuzi. Kwa kushinda tuzo hiyo, Kabunda atazawadiwa Sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania kesho.

Related

kimataifa 6703933715796758711

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii