Kagera yaipania Simba
 
http://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/kagera-yaipania-simba.html

Simba iliwasili Kagera mapema wiki hii, kuanza kusaka pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar.
Simba watakuwa na kibarua Kanda ya Ziwa, ikiwa baada ya mechi yao na Kagera ‘Wanankurukumbi’ itaingia Jijini Mwanza kuvaa Mbao na baadaye Toto Africans.
Jangalu, beki wa zamani wa Reli Morogoro, amesema kuwa Kagera Sugar haitakubali kirahisi kuruhusu pointi tatu dhidi ya Simba na kwamba amewaandaa vyema vijana wake kisaikolojia kuhakikisha wanashinda.
“Tumejiandaa vizuri, liwake jua au inyeshe mvua lazima tushinde. Simba ni timu nzuri, lakini hatuiogopi wala kuihofia tumewaandaa vijana kisaikolojia kuhakikisha haturuhusu pointi tatu,” amesema Jangalu.
