Kikosi cha timu ya taifa kutangazwa jumatatu

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/kikosi-cha-timu-ya-taifa-kutangazwa.html
Kocha wa muda wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' Salum Mayanga atatangaza wataalamu wa benchi la ufundi atakaofanya nao kazi Jumatatu ijayo. Tangu akabidhiwe jukumu la kuinoa Taifa Stars baada ya TFF kuvunja mkataba na Boniface Mkwasa, Mayanga hajawahi kutangaza wasaidizi wake. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Ofisa Habari wa Shirikisho hilo, Alfred Lucas amesema ataweka hadharani mikakati yake ya kiufundi. "Kocha pia atatangaza kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mchezo ya miwili ya kirafiki,"amesema Lucas. Kwa mujibu wa Lucas, Taifa Stars itacheza mechi za kirafiki dhidi ya Zambia na Rwanda na mchezo mmoja utachezwa hapa nchini na mwingine utapigwa ugenini. Wakati huohuo; Lucas amesema kikosi cha Serengeti Boys kitaingia kambini Jumapili hii kuanza maandalizi ya kushiriki fainali za Afrika kwa vijana. "Timu ikiingia kambini itakaa kwa muda mfupi na itakwenda Bukoba ambapo itacheza mechi za kujipima nguvu na Uganda, Burundi na Rwanda,"amesema Lucas. Aidha TFF imesema Serengeti Boys itakwenda Morocco Aprili 5 ambako itaweka kambi na kucheza mechi mbalimbali za kujipima nguvu. "Tumeomba mechi na Misri wamethibitisha kucheza nasi, lakini timu pia itakwenda Cameroon ambako itacheza mechi mbili na timu ya vijana ya nchi hiyo,"amesema Ofisa Habari huyo wa TFF.