Secta binafsi zailalamikia serikali

Uamuzi wa Serikali kuagiza wakala, taasisi za umma zianze kupewa kipaumbele cha kufanya biashara na Serikali yenyewe kwa lengo la kuziwezesha na kubana matumizi yake, unaiweka sekta binafsi katika wakati mgumu, hivyo kutishia kukua kwa uchumi wa nchi. Tangu Serikali ianze kutoa matamko yanayotaka mashirika na taasisi zake kufanya biashara baina yao, wamiliki wa biashara ya huduma kama hoteli, benki, usafirishaji na hata sekta ya nishati, sekta binafsi imekuwa katika hali ngumu. Baadhi ya wamiliki wa hoteli wamelazimika kuzifunga au kubadili matumizi ya majengo, benki zimelazimika kusimamisha baadhi ya huduma kama mikopo na baadhi ya wenye malori wamelazimika kuyaegesha. Tishio hilo linaonekana kuiwinda sekta ndogo ya nishati ambako Shirika la Umeme (Tanesco) linafanya kazi pamoja na kampuni binafsi ambazo baadhi zinachimba, kuchakata, kusafirisha na hata kuuza umeme baada ya Rais John Magufuli kusema wiki iliyopita kuwa kama kampuni binafsi zinataka kushiriki katika sekta hiyo hazina budi kuchimba, kusafirisha, kusambaza na kuuza umeme zenyewe badala ya kutumia mgongo wa Tanesco. Maamuzi ya Serikali yanayoendelea kutikisa sekta binafsi, yana historia ndefu. Habari zaidi soma Gazeti la Mwananchi.

Related

kitaifa 6909149701853230769

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii