Mahakama Tanga kusikiliza shauri la mjane






Mjane Swabaha Shosi.
Mjane Swabaha Shosi. 
 Unamkumbuka yule mjane aliyejitokeza mbele ya Rais John Magufuli mwezi Februari, kulalamikia mahakama na vyombo vingine vya dola kushindwa kutekeleza majukumu yake dhidi ya madai yake ya mirathi?
Leo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga itaanza kusikiliza utetezi wa Wakili Alfred Akaro baada ya kumuona ana kesi ya kujibu kuhusu shauri la kughushi wasia wa marehemu Mohamed Shosi lililofunguliwa na mjane huyo aitwaye
Swabaha Shosi.
Akaro alikuwa wakili wa Saburia Shosi ambaye ni mtoto wa marehemu katika kesi ya madai ya mirathi ya Mohamed Shosi iliyofunguliwa mahakamani hapo.
Katika shauri hilo la jinai namba 10/2016, mjane huyo anamlalamikia wakili huyo na Aboubakar Shaaban kwamba wameghushi wasia uliokuwa umeandikwa na Shosi kuhusu mirathi ya mali zake.
Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Aziza Lutala ametoa uamuzi wa shauri hilo baada ya kupitia malalamiko yaliyowasilishwa mahakamani na kusema ameona wakili hiyo ana kesi ya kujibu.



Related

kitaifa 5904694058898322796

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii