Mkuu wa mkoa akazia kaulimbiu ya viwanda

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/mkuu-wa-mkoa-akazia-kaulimbiu-ya-viwanda.html

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego
Katika kuhakikisha kuwa kaulimbiu hiyo inawaingia wawekezaji, Dendego amewataka watu walionunua viwanda serikalini kuvifufua badala ya kuvigeuza kuwa maeneo ya kutunzia korosho.
Dendego ametoa maelekezo hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau wa usimamizi wa msimu wa mauzo ya korosho kwa mikoa mitano.
Amesema kwamba kufufuliwa kwa viwanda hivyo kutasaidia kuongeza thamani ya zao hilo nchini kwa sababu
makubaliano ya Serikali na wamiliki hao yalikuwa ni kununua na kuviendeleza viwanda hivyo.
Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Hassan Jarufu amesema ufufuaji wa viwanda vya ubanguaji utawasaidia Watanzania wengi kunufaika kwa kupata ajira katika viwanda hivyo.