Mokiwa kavuliwa uongozi rasmi leo

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/mokiwa-kavuliwa-uongozi-rasmi-leo.html
Askofu Valentino Mokiwa amevuliwa uongozi wa kanisa la Anglikana katika Dayosisi ya Dar es Salaam. Akizungumza wakati wa ibada maalumu ya kuhitimisha mchakato wa kumtaka Mokiwa ajiuzulu leo, Askofu Mkuu wa Anglikana nchini, Dk Jacob Chimedeya amesema leo ndiyo mwisho wa mchakato huo na watu warudi makanisani mwao kuendelea na huduma za kiroho. Askofu Chimeledeya ameonya kwamba chochote kitakachoendelea baada ya ibada hiyo kitakuwa ni uvunjifu wa amani na kwamba ataviachia vyombo vya dola vifanye kazi yake. "Katiba yetu inatamka kwamba askofu wa dayosisi ni mmoja wa wadhamini wa kanisa. Kwa kuwa tumemvua uongozi Dk Mokiwa, natangaza kwamba yeye siyo mdhamini tena katika kanisa letu," amesema Dk Chimeledya.