Mtambo mpya wakupima vinasiba mbeya

Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali imejitanua baada ya kufunga mtambo mpya utakaohudumia mikoa ya kusini katika Jiji la Mbeya. Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele amesema lengo la kufunga mtambo huo aina ya Energy Dispersive X- Ray Fluorescence (ED-XRF), uliogharimu Sh200 milioni ni kurahisisha utendaji wao. Mtambo huo utapima sampuli za sumu pamoja na dawa za kulevya na una uwezo wa kupima na kutoa majibu ya aina zote za kemikali zilizopo kwenye sampuli kwa wakati mmoja. “Tumelenga mikoa hii na tumefunga mtambo huu Mbeya kwa kuzingatia kwamba kuna madini ya dhahabu, hivyo itakuwa rahisi zaidi kwa wafanyabiashara wa madini kuleta sampuli ya madini yao ili kuwasaidia ni aina gani ya dhahabu na ina kemikali kiasi gani,” alisema Pia, Profesa Manyele amesema mtambo huo utaisaidia kukabiliana na uhalifu wa makosa ya jinai na mambo mengine yanayohusu utambuzi wa mtu binafsi. Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, William Ntinika amesema kufungwa kwa mtambo huo kumewarahisishia wananchi muda na gharama ambazo walikuwa wakizitumia kufuata huduma hiyo jijini Dar es salaam.

Related

kitaifa 8937464989691534566

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii