Nyota wa zamani wa Liverpool mazoezini na under 15.dar

John Barnes, amewanoa wachezaji wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 katika siku yake ya kwanza nchini kuadhimisha miaka 100 ya benki ya Standard Chartered tangu kuanzishwa kwake. Mkali huyo alifanya hivyo juzi kwenye Uwanja wa JK Park uliopo Kidongo Chekundu, Dar es Salaam ambapo pia alipata fursa ya kubadilishana mawazo na Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Mholanzi Kim Poulsen. “Ni muhimu sana kuwafundisha vijana wadogo soka katika umri huu, viongozi wa soka Tanzania na wadau wote wa michezo ni vema kuweka nguvu zao za kutosha kwa vijana maana ni tegemeo la siku za usoni,” alisema Barnes. Katika ziara yake hiyo, Barnes pia alipata nafasi ya kushuhudia fainali ya timu tatu kutoka nchini za Tanzania, Uganda na Kenya ambazo zilipambana kuwania Kombe la Standard Chartered 2017 na hatimaye kushinda safari ya kuelekea Anfield mjini Liverpool. Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba, alisema kwamba timu ya Azania ya Tanzania ndiyo iliyoshinda safari ya Liverpool baada ya kuzishinda Capital Fm (Kenya) na Coca Cola (Uganda). “Tumeweza kumleta John Barnes kushiriki kwenye mazoezi ya vijana chini ya miaka 15 kwa ajili ya kuwaandaa kwenye mashindano ya AFCON ya vijana mwakani, lakini pia amekuja kwa ajili ya tukio la benki hiyo kutimiza miaka 100 tangu kuanza shughuli zake mwaka 1917 za kibenki nchini,” alisema Naye Kocha Poulsen, aliishukuru Standard Chartered kwa kufanikisha ujio wa gwiji hilo la soka kushiriki kwenye mazoezi na kutoa mchango wa mafunzo kwa vijana wake akiwataka wadau wengine wa michezo kuiga mfano wa benki hiyo kama chachu ya maendeleo ya soka kwa nchini zinazoendelea kama Tanzania.

Related

michezo na burudani 2303614853829372054

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii