Simba yaiombea mabaya yanga/azam

Simba wanafahamu kuwa wachawi wao katika harakati za kutwaa ubingwa msimu huu ni wapinzani wao wa jadi, Yanga kutokana na kuzidiana pointi chache, hivyo Wekundu wa Msimbazi hao kuamua kupiga magoti mchana na usiku ili Azam FC wafanye kweli dhidi ya Wanajangwani hao timu hizo zitakapokutana. Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wapo kileleni wakiwa na pointi 55 wakifuatiwa na Yanga wenye pointi 53, hiyo ikimaanisha kuwa wakongwe hao wamepishana kwa pointi mbili tu. Na sasa Wekundu wa Msimbazi wameungana na Azam kuhakikisha wapinzani wao hao wa jadi wanakufa kifo kibaya watakapokutana na Wanalambalamba hao. Simba ambayo ipo katika wakati mgumu, inatakiwa ifanye vizuri katika michezo yao mitatu ya Kanda ya Ziwa kwa kuzifunga Toto Africans, Mbao FC pamoja na Kagera Sugar kwa kujikusanyia pointi tisa ili kuipoka Yanga ubingwa ambao kwa sasa ni watetezi wa taji hilo. Licha ya kupambana kuhitaji pointi hizo, lakini pia inahitaji nguvu za ziada kutoka kwa Azam kuhakikisha anamzuia mpinzani wake anayewania nafasi hiyo kutokana na kumpita pointi mbili. Azam ambayo inahitaji kufanya vizuri katika michezo yake sita ili kujihakikishia nafasi ya tatu katika msimamo huo, italazimika kuifunga Yanga ili kujiongezea pointi za kumpeleka katika nafasi hiyo.

Related

michezo na burudani 8503644147038253563

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii