Serikali yaendelea kusisitiza ofisi kuamia dodoma.

   Jumla ya watumishi wa umma 2,059 wameripoti Dodoma katika awamu ya kwanza ya kuhamia mjini humo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais John Magufuli aliyoitoa wakati akikabidhiwa uenyekiti wa CCM, Julai 22, mwaka jana. Awamu ya kwanza ya Serikali kuhamia makao makuu Dodoma inajumuisha mawaziri na manaibu wao, makatibu wakuu na manaibu wao, baadhi ya wakurugenzi pamoja na wasaidizi wachache. Hayo yamebainishwa leo (Ijumaa) katika kikao cha kazi cha mawaziri na naibu mawaziri kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Hazina mjini Dodoma chini ya uwenyekiti wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Related

kitaifa 4919740681885820657

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii