Waziri mkuu wa ujerumani jibu tuhuma zinazomkabili

Angela Markel, amesema tuhuma zilizotolewa dhidi yake na Rais wa Uturuki, Recep Erdogan, kuhusu kuwaunga mkono magaidi hazina msingi wowote. Msemaji wa Kansela wa Ujerumani, Steffen Seibert, alibainisha kwamba Angela Merkel hana nia ya kushiriki katika michezo ya fitina. Rais Erdogan wa Uturuki juzi alimtuhumu Merkel kuwa anawaunga mkono magaidi, anawaficha nchini kwake na kukwamisha mapambano dhidi ya ugaidi. Siku za hivi karibuni maafisa wa miji kadhaa ya Ujerumani walifuta vikao vya uchaguzi vya maafisa wa chama tawala cha Uturuki, hatua iliyoikasirisha serikali ya Erdogan. Rais wa Uturuki amelinganisha hatua hiyo ya kufutwa vikao hivyo kuwa ni sawa na hatua za utawala wa Kinazi.

Related

kimataifa 6384904311367589684

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii