Fifa yabariki teknoloji kudhibiti makosa Kombe la Dunia



Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetangaza kutumia video kuwasaidia mwamuzi kutoa adhabu kwenye mashindano ya Kombe la Dunia mwakani.
Rais wa Fifa, Gianni Infantino alisema video hiyo itajumuisha timu mbalimbali zinazoshiriki na ratiba za mechi husika.
Mfumo huo tayari umeshafanyiwa majaribio nchini Italia, Uholanzi na Marekani na kuonyesha mafanikio mkubwa.
Bodi ya mashindano ya Kombe la Dunia imeelezea kwamba mfumo huo utamwezesha  mwamuzi kufanya uamuzi sahihi bila upendeleo kwa kila timu.
Mkurugenzi wa Bodi ya Kimataifa ya Soka (IFAB), David Elleray alithibitisha kwamba  mfumo huo utapunguza malalamiko kwa waamuzi na watafanya kazi zao kwa ufanisi zaidi, hata hivyo bado wanapokea mapendekezo kwa ajili ya kuboresha.
Alisema, “Tumefurahi mafanikio tuliyofikia. Tumekwenda hatua moja mbele. Tumegundua ni kwa namna gani tunaweza kuimarisha sekta ya michezo iwe bora zaidi.

Related

michezo na burudani 6774720086619053987

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii