Katiba ya Warioba yamtesa Polepole

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/04/katiba-ya-warioba-yamtesa-polepole.html

Polepole aliipigia debe la nguvu rasimu hiyo ambayo miongoni mwa mapendekezo yake ni uwapo wa Serikali tatu; Shirikisho, Tanzania Bara na Zanzibar.
Akizungumza juu ya rasimu hiyo Polepole alisema msimamo wake bado uko kwenye Rasimu ya Jaji Warioba.
“Msimamo wangu ndivyo ulivyo muda wote tangu mwanzo hata sasa na CCM inaamini hivyo, kuheshimu maoni ya wananchi,” alisema Polepole na kuongeza:
“Hatuwezi kupuuza watu kwa namna yoyote, CCM haiko hapa kupuuza watu bali kuwasikiliza na ndiyo maana msingi wa mageuzi ya chama ni kuwa cha wanachama, unapokuwa na chama cha wanachama unakuwa daraja kati ya wananchi na Serikali.”
Kuhusu utawala wa Rais John Magufuli kwa suala la Katiba, alisema kumekuwa na mageuzi yanayofanywa kabla ya kufikia kwenye mchakato wa Katiba.