Arsenal yairudisha Man United sita




Ushindi wa Arsenal wa mabao 2-0 dhidi ya Southampton umeishusha Manchester United hadi nafasi ya sita.
Mabao ya Alex Sanchez na Oliver Giroud yaliipandisha Arsenal hadi nafasi ya tano jambo linalowapa jeuri ya kuwania nafasi nne za juu kwenye ligi hiyo inayoelekea ukingoni.
Southampton walionekana kuwa dhaifu mbele ya Arsenal  ambao walifanya mashambulizi ya mara kwa mara.
Ushindi huo umefanya kuwapo tofauti ya pointi tatu kati ya Arsenal na Man City iliyojikita nafasi ya tatu.
Kocha Arsene Wenger amefufua matuamini ya kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao, tangu alipoibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester United wiki iliyopita.
Arsenal sasa wamefikisha pointi 66 huku Chelsea yenye pointi 84 ikisubiri kutawazwa bingwa iwap itafanikiwa kuifunga West Brom kwenye mchezo wao wa Ijumaa.

Related

michezo na burudani 4915306868944937825

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii