CAF yasaka vijeba Serengeti Boys




Zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya kuanza kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana, Gabon,  Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limefanya vipimo MRI kwa wachezaji wa timu zinazishiriki fainali hizo.
Vipimo hivyo ni maalumu kwa ajili ya kutambua umri wa wachezaji hao.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi alisema CAF ilifanya vipimo hivyo juzi na inatarajia kutoa majibu wakati wowote.
"Wameshapimwa na tunasuburi majibu wakati wowote, nikijulishwa nitakwambia,"alisema Malinzi alipohojiwa na mtandao huu.
Serengeti Boys imepangwa Kundi B katika fainali hizo ikiwa na timu za Mali, Angola na Niger na inatarajia kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Mali

Related

michezo na burudani 8156129128748723869

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii