Banda ajitangaza kuikacha Simba na kujiunga na Baroka FC ya Sauzi
http://maisharaisi.blogspot.com/2017/07/banda-ajitangaza-kuikacha-simba-na.html
Banda amemaliza mkataba wake na Simba mwezi uliopita alitangaza kuondoka kwenye timu hiyo kabla ya mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Mbao mwishoni mwa mwezi wa Mei mwaka huu.
Hata hivyo, uongozi wa Simba ulikaa naye na kufanya mazungumzo yaliyofanikisha adhma yake ya kusaini mkataba na timu hiyo, lakini kwa sharti kwamba akipata timu yoyote wakati wowote ataondoka.
Wakati taarifa zikidai hakuwa amesaini mkataba huo wakati anaondoka na timu ya Taifa Stars kushiriki mashindano ya Cosafa imezua sintofahamu juu ya beki huyo kufichua kuwa atakuwa mchezaji wa Baroka FC msimu ujao.
Banda alitumia akaunti yake Instagram kuthibitisha kwamba kwa sasa ni mchezaji mpya wa Baroka.
Endapo atajiunga na timu hiyo Banda atakuwa amefuata nyayo za wachezaji wawili wa ukanda huu wa Afrika Mashariki kuichezea timu hiyo wengeni ni Khalid Aucho wa Kenya na Geffrey Massa wa Uganda.
